Jumatano, 9 Novemba 2016

HUYU NDIYE YULE ASKARI FEKI ALIYEKAMATWA MWANZA.




AKAMATWA AKISAFIRISHA MAITI KWA PIKIPIKI.

Huyu ndiye yule jamaa aliyekamatwa akisafirisha maiti kwa pikipiki baada ya familia ya marehemu kutokua na uwezo wa kusafirisha.

AGONGA GARI LA POLISI AKIJIPIGA SELFIE

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha nchini Marekani aligongesha gari lake kwa lile la polisi wakati akijipiga selfie huku akiendesha gari.

Miranda Rader mwenye umri wa miaka 19,aliligonga gari la polisi alipokua akimtumia picha za utupu mpenzi wake kupitia mtandao wa Snapchart.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Bryan umbali wa km 160 kaskazin mwa mji wa Houston,ilisababisha mfuko wa hewa kuchomoka.
Alikamatwa kwa kushukiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa na kuachiwa kwa dhamana ya dolla 2000.

PICHA:HILLARY CLINTON,NA TRUMP WAKIWA WATOTO.



MAMBA MKUBWA AKAMATWA NA KUACHIWA SRI LANKA.

Mamba mkubwa mwenye urefu wa futi 17 amekamatwa eneo la Matara,Sri lanka.Mamba huyo alikua amekwama kwenye mfereji unaosafirisha maji hadi mto NILWALA.
Alisafirishwa na kuachiwa huru na maafsa wanyama pori.

CLINTON AKUBALI KUSHINDWA.

Mgombea wa urais nchini Marekani bwn,Donald Trump amemshinda bi. Hillary Clinton wa chama cha Democratic.
Trump alishinda majimbo mengi yaliyokua yanashundaniwa.Trump amepata kura 278 za wajumbe wakati Clinton alipata kura 218.
Baada ya matokeo kutangazwa bi. Clinton alimpigia simu Trump na kumpongeza kwa ushindi huo.

Jumamosi, 5 Novemba 2016

PICHA:AKAA KWENYE JENEZA SIKU NZIMA ILI AZOEE KIFO.




KIFO CHA MUUZA SAMAKI CHAZUA MAANDAMANO MOROCCO.

Maelfu ya raia wa Morocco juzi walifanya maandamano katika miji kadhaa baada ya muuza samaki mmoja kugongwa na gali la kubebea takataka hadi kufa alipojaribu kuchukua samaki wake ambao alipokonywa na maafsa wa Polisi.
Kifo cha Maouhcine Fikri katika mji wa kaskazini wa Al Houciema siku ya Ijumaa kilizua hasira kali miongoni mwa raia katika mitandao ya kijamii.
Mfalme wa Morocco king Mohammed amewaagiza maafsa kutembelea familia ya Fikri.

TRUMP:CLINTON ATAANZISHA VITA KUU YA TATU YA DUNIA.

Mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic bw.Donald Trump amesema mpango wa mpinzani wake Hilary Clinton kuhusu kutatua mzozo wa SYRIA UTAANZISHA VITA KUU YA TATU YA DUNIA.
Amesema Marekani inafaa kuangazia zaidi kushinda vita dhidi ya kundi la ISLAMIC STATE badala ya kulenga kumshawishi au kumshinikiza Rais wa SYRIA Bashar Assad kungatuka uongozini.
Bwn.Trump pia amewashambulia wafuasi na na viongozi wa Republican ambao wamekataa kumuunga mkono...

MWANAMKE MWENYE MACHO YA KUSHANGAZA AFUNGWA JELA.

Mhamiaji kutoka AFGHANISTAN ,ambaye alipata umaarufu picha yake ilipochapishwa kwanza katika jarida la National Geographic miaka thelathini iliyopita amekamatwa.
Maafisa wamesema amekamatwa kwa kua na nyaraka bandia za vitambulisho.
Sharbat GULA alipata umaarufu mwaka 1985 kutokana na piha hiyo iliyopigwa akiwa na umri wa miaka 12.Macho yake yalikua na rangi ya kijani jambo amabalo lilifanya kufahamika kwa jina la GREEN EYED GIRL.
Maafisa wanasema alikamatwa na idara ya uchunguzi ya Pakistani(FIA) baada ya kuwasilisha maombi ya kitambulisho akitumia jina la SHARBAT BIBI.

MAPYA YAIBUKA KIFO CHA THOMAS MASHALI.

Tasnia ya michezo nchini hivi majuzi ilipata pigo baada ya kumpoteza bondia Thomas MASHALI ambaye alifariki baada ya kupigwa na watu wasio julikana.Akiongea na blog hii Shuhuda wa tukio hilo alisema Mashali alikwenda KIMARA kwa ajili kudai pesa yake kwa mtu ambaye alimkopesha.
Aiongea alisema ..Tulikua wote mpaka jioni aliponiambia anakwenda kimara kudai pesa yake kwa mtu ambaye alimuuzia simu aina ya smartphone hivyo alikwenda kdeni lake lililobaki.
Akiongea baba yake mzazi alisema hakuwahi kuhudhulia hata pambano moja la Mashali na hawakuwahi kuonana kwa miezi mitatu mpaka alipotoweka duniani.
Ikumbukwe Thomas Mashali alifariki baada ya kupigwa na mapanga na vitu vyenye ncha kali na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Muhimbili.

HUU NDIO WIMBO MPYA WA ALI KIBA NA OMMY DIMPOZ.

Mkali wa bongo Fleva Ali kiba amefunguka na kusema wazi juu ya ujio wa wimbo mpya ambao amemshirikisha Ommy Dimpoz uiitwao KAJIANDAE.
Kiukweli ni wimbo mzuri pili maandaizi ya video tumeshafanya na jina la wimbo unaitwa Kajiandae,So mashabiki wangu na mashabiki wa Ommy Dimpoz wakati wowote watatpata radha nzuri tu kwani najua ni kitu gani mashabiki wa mziki wangu wanachotaka kutoka kwangu..Alisema ALI KIBA.

MSUNGO WA MADEBE YUPO MADUKANI

Baada ya kusambaa kwa picha kadhaa zikionesha watu wakiwa katika kaburi lenye jina la Madebe Lidai,na madebe mwenyewe kutueleza kuwa haikua kweli amefariki bali ni katika upigaji picha wa filamu mpya,sasa filamu hiyo iko madukani.
Akiongea na mimi Madebe amesema <<<ni kweli kaka nilikua katika upigaji picha ya filamu yangu inayoitwa msungo na kila kitu kipo sawa na sasa mzigo upo sokoni.
Ikumbukwe Madebe Lidai ndiye msanii anayekuja ka kasi nchi kwa sasa baada ya kutamba na filamu yake ya KASUMBA,NOMGWA,MAKAME nk.
Mmoja ya washiriki wa filamu hiyo ya MSUNGO ambayo iko madukani kwa sasa.
 
Madebe Lidai

Jumatatu, 24 Oktoba 2016

BIEBER AONESHA JEURI YA PESA.

Wakati wewe unawaza utakula nini mwingine anafikilia atatumia vipi,hilo amedhihirisha Justin Bieber kwa kupangisha nyumba ya kifahari North London kwa kile alichodai kufurahia mazingira ya neneo hilo.
Kwa mujibu wa Dily mail licha ya kulikodi kwa Euro 1.3 mil. Bieber hata hamishia maisha yake kwenye jumba hilo bali atakua akitembelea mara kadhaa kutokana na kuvutiwa na mazingira.
Jumba hilo linatajwa klua na vyumba 15 vya kulala,ukumbi wa sinema,bwawa la kuogelea na baa.

BABU TALE AKOMALIWA MAHAKAMANI.

Mkurugenzi wa kampuni ya Tip top connection ya jijini dar es salaam,Hamis Shabani maarufu kama Babu Tale amekwama tena mahakamani katika harakati zake za kukwepa ulipaji wa fidia ya mamilioni kutokana na makosa ya haki miliki.
Babu Tale ambaye pia ni meneja wa Daimond platinum alikwama baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake.
Alipaswa aileze mahakama kwanini asifungwe  kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama iliyoamuru kulipa fidia ya mil.250 baada ya kupatikana na hatia ya ukiukwaji wa sharia ya haki miliki.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mhadhiri wa dini ya Kiislam, Sheikh Hashim Bonde kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ya ridhaa yake.-----MWANANCHI.
BABU TALE
 

WASTARA NA MATUSI.

Wasanii wanatazamwa kama kioo cha jamii,kwa maana hiyo wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na watu wanao watazama,hata hivyo maisha wanaoishi baadhi ya wasanii hao hayaakisi msemo huo.
Miongoni mwa mambo yanayofanywa ambayo ni kinyume na matarajio ni kutoa maneno machafu live au kutumia mitandao ya kijamii.
Wastara Juma ni miongoni mwa wasanii wanao heshimika katika jamii na ni msanii wa kike ambaye anaweza kusimama\ na kusema na kusikilizwa kwa jinsi alivyokua amejiweka.
Kataika siku za hivi karibuni alichafuka baada ya kuingia majaribuni na kuingia katika orodha ya wasanii wanaotukana mitandaoni baada ya kumvaa mmoja wa mashabiki wake aliyemsemea mbovu na kumtukana.
Chanzo cha yote hayo ni baada ya Wastara kuweka picha katika akaunti yake ya Instagram ambayo amemlalia kifuani mpenzi wake Bond bin Sinan na mashabiki wake kuanza kumzodoa.

Watara juma.

LULU ACHUKIZWA NA TATOO YAKE.

Unapozungumzia tattoo kwa wasanii wa nje inawezekanaLil wayne anaongoza kwa kua na michoro mingi mwilini mwake,mpaka sasa anamichoro 300.
Uchoraji kwa tattoo kwa wasanii wa bongo pia wamekua nazo zaidi ya moja.
Elizabert Michael(LULU) anasema anazo nyingi lakini zinazoonekana nyingi ni tatu,huku akidai kati ya zote zilizopo mwilini mwake ipo moja inayomchukiza.
''Niliichora lakini kwa sasa sitaki hata kuiona na kufuta ni shighuri hivyo nabaki kua nayo bila ya sababu wala maana nayo,zilizo baki zote zina maana'' alisema Lulu.
Only God can Judge me,ndio unavyosomeka mchoro huo uliopo chini kidogo ya shingo yake.
Elizabert  Michael(LULU)

MADEBE LIDAI ALIZA WATU.

Sanaa ni uwezo na ubunifu wa msanii katika kuwasilisha mawzo na fikra zake kwa hadhira kwa kutumia ubunifu.Tukija katika tasnia ya filamu nchini wasanii wengi wa bongo wamekosa ubunifu na hii inatokana na ufinyu wa bajeti ama mawazo ya msanii husika.
Madebe lidai ni msanii anayekuja kwa kasi katika suala Zima la ubunifu na hivi karibuni ameibua sintofahamu kwa mashabiki wake baada ya kupost picha ya kabuli lililoandikwa jina lake katika ukurasa wake wa facebook.
Akiitolea ufafanuzi picha hiyo madebe alisema...>>kwa sasa nipo katika utengenezaji wa film yangu hiyo na mashabiki wangu wasiwe na wasiwasi mimi niko hai na naendelea na kazi zangu za sanaa na hiyo picha ni moja ya clip ambazo zipo katika film hiyo..
 
Watu wakiomba dua katika kaburi la Madebe lidai ndani ya film hiyo huku mashahidi yakiandikwa jina la madebe lidai

Ijumaa, 21 Oktoba 2016

CASSO BENZEMA ATAMBULISHA NGOMA MPYA

Msanii mkongwe katika tasnia ya bongo movie Rose Ndauka jana amemtamulisha kwa mara ya kwanza msanii wake ambaye yuko chini ya lebo yake ya NDAUKA ADVERTS.Akiongea mbele ya waandishi wa habari ofisinin kwake SINZA..Rose alisema anamtambulisha CASSO baada ya kumuandaa kwa muda mrefu ili aje kua msanii mkubwa hapo siku za baadae.Wimbo huo ambao umerekodiwa kwa producer man water mpaka sasa upo katika MKITO.COM hivyo nawaaomba mashabiki wangu wanipokee na wanipe sapoti...aliongeza CASSO.


MISS KATOTO:KAZI KWANZA,MAPENZI BAADAE

Model anayekuja kwa kasi katika tasnia ya mitindo nchini Miss katoto amesema kazi kwake ndio kila kitu kwa sasa na hataki kuchanganya na Mapenzi.Akiongea wakati wa upigaji wa picha ambazo zitatumika katika moja ya jarida la mitindo nchini alisema...Kwa sasa naangalia kazi ambayo itanipatia mkwanja mrefu,..mpka sasa mimi nifanya kazi kadhaa ambazo bado hazijatoka na pindi zitakapotoka basi naamini watu watanielewa vizuri so Nimefanya kama Video queen katika video za wasani kadhaa wa bongo fleva na Mtangazo ya biashara.

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

WANASAYANSI KUUNDA TAIFA JIPYA ANGA ZA JUU.

Kundi la wanasayansi mjini Vienna,Australia wameanza mpango wa kuunda taifa jipya na la aina yake ambalo litaitwa ASGARDIA.Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo ambalo litakua katika anga za juu katika mzingo wa Dunia eneo ambalo vyombo vya anga huzunguka dunia.Wanasayansi hao wanapanga kurusha Satelaiti ya kwanza ya kuanzisha Taifa hilo mwishoni mwa mwaka ujao.Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja watatambuliwa na umoja wa mataifa.Tayari mpaka sasa watu50,000wamewasilisha maombi mtandaoni kuwa raia wa taifa hilo_BBC.

MWALIMU AUA MWANAFUNZI KWA FIMBO.

Mwanafunzi David Ngangu mwenye umri wa miaka 14 amefariki dunia baada ya kupokea kipigo kutoka kwa mwalimu wake baada ya kufeli somo la maarifa ya jamii.Mwanafunzi huyo ambaye alikua akisoma darasa la 8 katika shule ya msingi Subukia nchini Kenya alifariki saa chache baada ya kipigo.Mama mzazi wa mwanafunzi huyo alisema mtoto huyo alilalamika maumivu ya kichwa kutokana na kipigo cha mwalimu kisa ikiwa ni kufeli na kushidwa kufika wastani wa somo la maarifa ya jamii_The starndard

NCHI ZINAZOONGOZA KUA NA WANAFUNZI WENYE AKILI ZAIDI DUNIANI.

Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka Marekani na Uengereza kama vile Harvard,MIT,Stanford,Oxford, CAMBRIGDE etc.Lakini baada ya Shirika la kimataifa la Uchunguzi wa maendeleo(OECD) kuchunguza uwezo wa kusoma na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu Duniani wanafunzi walio bora zaidi wanatoka Japan na Finland na wala sio Marekani na Uengereza.Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanao hitimu kwa mujibu wa OECD ni 1.JAPAN,2.FINLAND,3.UHOLANZI,4.AUSTRALIA,5.NORWAY,6.UBELGIJI,7.NEW ZEALAND,8.ENGLAND,9.MAREKANI,10.JAMHURI YA CZECH.

SAIDI:NIMETOLEWA MACHO, SI AKILI.

Kijana aliyeshambuliwa na kutolewa macho usiku wa septemba 6 akiwa buguruni jijini Dar es salaam na habari zake kutawala katika vyombo vya habari na mitandao bw. Saidi ALLY amesema kutolewa macho sio mwisho wa maisha yake.>>Nashukuru nimepata misaada mbalimbali kutoka kwa wadau na kwa kua imekuja kama mitaji, Nitasimamia biashara hiyo nikishirikiana na mke wangu pamoja na ndugu zangu.Nina imani nitaishi mpaka siku Mungu aliyoniandikia kua nitaondoka Duniani,..Nimetolewa macho,si akili nitahakikisha vitu nilivyopewa vitatumika kwa manufaa na familia yangu na nitahakikisha inaishi maisha ya kawaida. Binafsi naamioni Mungu ndiye muwez wa yote na hakuna linalomshinda,hivyo sijakata tamaa naamini nitaona na maisha yataendelea kama kawaida.

Jumanne, 18 Oktoba 2016

FORBES :DAIMOND NDIYE MSANII TAJIRI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI.

Jarida la Forbes la Nchini Marekani limetoa orodha ya wasanii matajili Duniani, Afika na katika kanda mbalimbali ambapo kwa upande wa Afrika mashariki Daimond Platnum ameongoza kwa kua na utajili wa Dolla mil.4.5 ambao ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania hasa baada ya kununua jumba la kifahari nchini Afrika kusini.Vitu vingine ambavyi Chibu dangote kama anavyofahamika na mashabiki wake ambavyo anamiliki ni pamoja na Majumba ya kifahari dar es salaam, Magari ya kifahari,Berber shop na maduka mbalimbali ya nguo za kisasa na mitindo na vingine vingi.Kwa Afrika mashariki daimond amefatiwa na Dr.Jose chamilion wa Uganda mwenye utajili unaokadiliwa wa dola mil.3.9..Wnafuata Akothee na Jaguar anashika nafasi ya nne.Wnachokiangalia jarida la Forbes sio pesa anazomiliki msanii katika akaunti zake bali ni thamani ya vitu anavyomiliki.

POGBA KINARA WA MAUZO YA JEZI EPL.

Kwa mujibu wa takwimu za SPORTS DIRECT staa mpya katika club ya Manchester united Poul POgba ambaye aliweka rekodi katika uhamisho wake katika dirisha lililopita ndiye anayeongoza kwa mauzo ya jezi kwa sasa kuliko staa yeyote yule.Dullahmasende.blogspot.com inakuletea mastaa 10 ambao wanaongoza kwa mauzo ya jezi.1.POGBA 2.IBRAHIMOVIC 3.ALEXIS SANCHEZ 4.MESUT OZIL 5.PHILIPE COUTINHO 6.DAVID DE GEA 7.SADIO MANE 8.DIMITRI PAYET 10.MARCUS RASHFORD.

Jumatatu, 17 Oktoba 2016

TANGULIA MWALIMU SCORPION

Tukio la kijana Saidi Ally ambaye aliyetobolewa macho wiki kadhaa na mtu aliyefahamika kwa jina la SCORPION katika maeneo ya Buguruni sheli jijini dar es salaam lilizua mijadala mingi mitandaoni.Hali hiyo ilipelekea msanii ENOCK MICHAEL kuigiza kipande cha video chenye kuhusiana na tukio hilo na kupewa jina la mwalimu scorpion.Kwa habari ambazo hazijathibitishwa ni kwamba kijana Enock amepata ajali mbaya ya Pikipiki na kufariki papo hapo,Endelea kufuatilia Dullahmasende.blogspot.com ili kujua undani wa taarifa hiyo.