Alhamisi, 20 Oktoba 2016

WANASAYANSI KUUNDA TAIFA JIPYA ANGA ZA JUU.

Tags

Kundi la wanasayansi mjini Vienna,Australia wameanza mpango wa kuunda taifa jipya na la aina yake ambalo litaitwa ASGARDIA.Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo ambalo litakua katika anga za juu katika mzingo wa Dunia eneo ambalo vyombo vya anga huzunguka dunia.Wanasayansi hao wanapanga kurusha Satelaiti ya kwanza ya kuanzisha Taifa hilo mwishoni mwa mwaka ujao.Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja watatambuliwa na umoja wa mataifa.Tayari mpaka sasa watu50,000wamewasilisha maombi mtandaoni kuwa raia wa taifa hilo_BBC.


EmoticonEmoticon