Jumamosi, 15 Oktoba 2016

MADEBE MGENI MUALIKWA KATIKA USIKU WA MOYO WA SHETANI LEO.

Tags
Utaratibu wa kuzindua filamu pindi inapokwisha umekua ni kitu cha kawaida sana kwa wasanii wakubwa wa Bongo movies.Lakini kwa wasanii wachanga kufanya kitu kama hiko imekua ni nadra sana  katika tasnia ya film nchini.Kampuni ya SCHIEDAM MEDIA leo inazindua filamu yao iliyochezwa na wasanii wachanga tupu,nasema haya ni maendeleo kwani ni wasanii wachache ambao wanaweza kufanya kitu kama hiko.Akiongea na dullah masende blog mmoja wa waratibu wa shughuri hiyo ambaye pia ni director katika film hiyo AMANZY MOHAMMED amesema kila kitu kipo tayari na maandalizi yote yamekamilika na show itaanza saa kumi kamili jioni,aliongeza Amanzy  mbali na uzinduzi wa filamu pia kutakua na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa bongo fleva na Singeli.Pia kutakua na burudani kutoka kwa DRAMA BOY, papaa Masai pamoja na kundi zima la the Chocalate team,Yaani watu w
aje tu waone tumefanya nini katika film hiyo ambayo Mgeni rasmi atakua mh.ABDALLAH MTOLEA mbunge wa TEMEKE alisema.Tuko vizuri kaka na mgeni rasmi atakua mbunge wetu a temeke.Tukio hilo litasindikizwa na wasanii mbalimbali wa bongo movie kama vile MSHINDO JUMANNE na MADEBE LIDAI..,Pia amedokeza Amanzy kua SHOW itafanyika katika UKUMBI wa LUPINGU PUB uliopo YOMBO DOVYA na kiingilio kitakua 2000/=tu.

TOFAUTI YA MADEBE LIDAI NA WASANII WENGINE WA BONGO MOVIES

Tags
Soko la tasnia ya Filamu nchini limeendelea kudorora kila siku iendayo kwa MUNGU. Na hii imetoana na kile kinachoitwa unyonyaji wa Wasambazaji wa Film nchini.Kutokana na kushuka huku kwa soko la filamu inayopelekea waandaaji wa kazi hizo za sanaa kutumia nguvu nyingi katika kuandaa kazi zao na malipo huwa kiduchu.Akipiga story na DULLAH MASENDE BLOG director wa movies za kibongo nchini ENOCK MSUMA amesema suala la kushuka kwa soko la filamu nchini limetokana na wasanii wakongwe kutokua wabunifu na pia kuwanyima nafasi ya kuonesha vipaji vyao wasanii wachanga katika kazi zao.Yaani hawa jamaa wanaogopa kufunikwa na underground na ndio maana hawataki kuwashirikisha katika kazi zao,alisema ENOCK. Akimtolea mfano MADEBE LIDAI anasema ENOCK kua mtazame MADEBE yuko kivyake sana na kazi zake zinaenda vizuri na hii imetokana na Madebe kujielewa na kutokua na mawazo ya kutolewa na mastaa ambao wanajiona wao ni wao na hawataki kuwasikiliza wasanii wachanga pindi wanapowaita katika kazi zao.Akiendelea kusema msuma...Yaani kaka soko limeshuka ni kutokana na hao wanaojiita mastaa kutokua wabunifu sasa unafikiri MUHINDI atanunua kazi mbovu? alihoji Msuma....na hawataki kuwashirikisha wasanii wachanga kwa kuhofia kufunikwa kwani wasanii wachanga wana kiu ya kufanikiwa hivyo wanapopata nafasi wanaitumia kikamilifu.Madebe lidai ni msanii ambaye amefanya kazi nyingi ikiwemo KASUMBA,NONGWA,MAKAME na nyinginezo.Akiongea na blog hii amesema anasambaza Kazi zake mwenyewe baada ya kugundua kufanya hivyo kuna faida kubwa kul
Madebe lidai(kushoto) akiwa katika moja ya kazi yake mpya
iko kwenda kummuzia MUHINDI.