Jumatatu, 24 Oktoba 2016

BABU TALE AKOMALIWA MAHAKAMANI.

Tags

Mkurugenzi wa kampuni ya Tip top connection ya jijini dar es salaam,Hamis Shabani maarufu kama Babu Tale amekwama tena mahakamani katika harakati zake za kukwepa ulipaji wa fidia ya mamilioni kutokana na makosa ya haki miliki.
Babu Tale ambaye pia ni meneja wa Daimond platinum alikwama baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake.
Alipaswa aileze mahakama kwanini asifungwe  kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama iliyoamuru kulipa fidia ya mil.250 baada ya kupatikana na hatia ya ukiukwaji wa sharia ya haki miliki.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mhadhiri wa dini ya Kiislam, Sheikh Hashim Bonde kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ya ridhaa yake.-----MWANANCHI.

BABU TALE
 


EmoticonEmoticon