Jumatatu, 24 Oktoba 2016

WASTARA NA MATUSI.

Tags

Wasanii wanatazamwa kama kioo cha jamii,kwa maana hiyo wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na watu wanao watazama,hata hivyo maisha wanaoishi baadhi ya wasanii hao hayaakisi msemo huo.
Miongoni mwa mambo yanayofanywa ambayo ni kinyume na matarajio ni kutoa maneno machafu live au kutumia mitandao ya kijamii.
Wastara Juma ni miongoni mwa wasanii wanao heshimika katika jamii na ni msanii wa kike ambaye anaweza kusimama\ na kusema na kusikilizwa kwa jinsi alivyokua amejiweka.
Kataika siku za hivi karibuni alichafuka baada ya kuingia majaribuni na kuingia katika orodha ya wasanii wanaotukana mitandaoni baada ya kumvaa mmoja wa mashabiki wake aliyemsemea mbovu na kumtukana.
Chanzo cha yote hayo ni baada ya Wastara kuweka picha katika akaunti yake ya Instagram ambayo amemlalia kifuani mpenzi wake Bond bin Sinan na mashabiki wake kuanza kumzodoa.


Watara juma.


EmoticonEmoticon