Jumatatu, 24 Oktoba 2016

BIEBER AONESHA JEURI YA PESA.

Tags
Wakati wewe unawaza utakula nini mwingine anafikilia atatumia vipi,hilo amedhihirisha Justin Bieber kwa kupangisha nyumba ya kifahari North London kwa kile alichodai kufurahia mazingira ya neneo hilo.
Kwa mujibu wa Dily mail licha ya kulikodi kwa Euro 1.3 mil. Bieber hata hamishia maisha yake kwenye jumba hilo bali atakua akitembelea mara kadhaa kutokana na kuvutiwa na mazingira.
Jumba hilo linatajwa klua na vyumba 15 vya kulala,ukumbi wa sinema,bwawa la kuogelea na baa.

BABU TALE AKOMALIWA MAHAKAMANI.

Tags
Mkurugenzi wa kampuni ya Tip top connection ya jijini dar es salaam,Hamis Shabani maarufu kama Babu Tale amekwama tena mahakamani katika harakati zake za kukwepa ulipaji wa fidia ya mamilioni kutokana na makosa ya haki miliki.
Babu Tale ambaye pia ni meneja wa Daimond platinum alikwama baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake.
Alipaswa aileze mahakama kwanini asifungwe  kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama iliyoamuru kulipa fidia ya mil.250 baada ya kupatikana na hatia ya ukiukwaji wa sharia ya haki miliki.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mhadhiri wa dini ya Kiislam, Sheikh Hashim Bonde kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ya ridhaa yake.-----MWANANCHI.
BABU TALE
 

WASTARA NA MATUSI.

Tags
Wasanii wanatazamwa kama kioo cha jamii,kwa maana hiyo wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na watu wanao watazama,hata hivyo maisha wanaoishi baadhi ya wasanii hao hayaakisi msemo huo.
Miongoni mwa mambo yanayofanywa ambayo ni kinyume na matarajio ni kutoa maneno machafu live au kutumia mitandao ya kijamii.
Wastara Juma ni miongoni mwa wasanii wanao heshimika katika jamii na ni msanii wa kike ambaye anaweza kusimama\ na kusema na kusikilizwa kwa jinsi alivyokua amejiweka.
Kataika siku za hivi karibuni alichafuka baada ya kuingia majaribuni na kuingia katika orodha ya wasanii wanaotukana mitandaoni baada ya kumvaa mmoja wa mashabiki wake aliyemsemea mbovu na kumtukana.
Chanzo cha yote hayo ni baada ya Wastara kuweka picha katika akaunti yake ya Instagram ambayo amemlalia kifuani mpenzi wake Bond bin Sinan na mashabiki wake kuanza kumzodoa.

Watara juma.

LULU ACHUKIZWA NA TATOO YAKE.

Tags
Unapozungumzia tattoo kwa wasanii wa nje inawezekanaLil wayne anaongoza kwa kua na michoro mingi mwilini mwake,mpaka sasa anamichoro 300.
Uchoraji kwa tattoo kwa wasanii wa bongo pia wamekua nazo zaidi ya moja.
Elizabert Michael(LULU) anasema anazo nyingi lakini zinazoonekana nyingi ni tatu,huku akidai kati ya zote zilizopo mwilini mwake ipo moja inayomchukiza.
''Niliichora lakini kwa sasa sitaki hata kuiona na kufuta ni shighuri hivyo nabaki kua nayo bila ya sababu wala maana nayo,zilizo baki zote zina maana'' alisema Lulu.
Only God can Judge me,ndio unavyosomeka mchoro huo uliopo chini kidogo ya shingo yake.
Elizabert  Michael(LULU)

MADEBE LIDAI ALIZA WATU.

Tags
Sanaa ni uwezo na ubunifu wa msanii katika kuwasilisha mawzo na fikra zake kwa hadhira kwa kutumia ubunifu.Tukija katika tasnia ya filamu nchini wasanii wengi wa bongo wamekosa ubunifu na hii inatokana na ufinyu wa bajeti ama mawazo ya msanii husika.
Madebe lidai ni msanii anayekuja kwa kasi katika suala Zima la ubunifu na hivi karibuni ameibua sintofahamu kwa mashabiki wake baada ya kupost picha ya kabuli lililoandikwa jina lake katika ukurasa wake wa facebook.
Akiitolea ufafanuzi picha hiyo madebe alisema...>>kwa sasa nipo katika utengenezaji wa film yangu hiyo na mashabiki wangu wasiwe na wasiwasi mimi niko hai na naendelea na kazi zangu za sanaa na hiyo picha ni moja ya clip ambazo zipo katika film hiyo..
 
Watu wakiomba dua katika kaburi la Madebe lidai ndani ya film hiyo huku mashahidi yakiandikwa jina la madebe lidai