Jumamosi, 17 Septemba 2016

ALI KIBA,DAIMOND USO KWA USO SAUZ

Tags
Wasanii nguli nchi ambao wana upinzani mkubwa ALI KIBA na DIAMOND PLATNUM wanataraji kupanda jukwaani jijini Johanesburg Afrika kusini katika Tamasha la utoaji wa Tuzo za MTV Africa music Awards.Tnzo hizo ambazo zitaoneshwa moja kwa moja kupitia dstv katika chanel zake za MTV base na MTV.Hiyo ni nafasi ambayo wataipata wasanii hao kuoneshana ubabe wa nani mkali kati yao.Ikumbukwe tu hivi majuzi Ali kiba alikua mjini mombasa Kenya amabapo alifanya show pamoja na Msanii kutoka Marekani CRISS BROWN,katika tamasha hilo liliingia doa kwa ALI KIBA baada ya kudai kuzimiwa mic na Meneja wa Daimond.Mkurugenzi mtendaji wa Multchoice Tanzania bwna. Maharage Chande alisema mbali ya kutoa burudani katika show hiyo pia wasanii hao watakua katika kinyang`anyiro cha kuwania tuzo.Alidokeza pia ukiacha wasanii hao pia Tanzania itawakilishwa na Vanessa Mdee,Rayvany,Yamoto band na Navy Kenzo ambao watashiriki katika kuwania Tuzo mbalimbali hivyo kuwataka watanzania kuwaunga mkono wasanii hao.