Alhamisi, 20 Oktoba 2016

WANASAYANSI KUUNDA TAIFA JIPYA ANGA ZA JUU.

Tags
Kundi la wanasayansi mjini Vienna,Australia wameanza mpango wa kuunda taifa jipya na la aina yake ambalo litaitwa ASGARDIA.Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo ambalo litakua katika anga za juu katika mzingo wa Dunia eneo ambalo vyombo vya anga huzunguka dunia.Wanasayansi hao wanapanga kurusha Satelaiti ya kwanza ya kuanzisha Taifa hilo mwishoni mwa mwaka ujao.Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja watatambuliwa na umoja wa mataifa.Tayari mpaka sasa watu50,000wamewasilisha maombi mtandaoni kuwa raia wa taifa hilo_BBC.

MWALIMU AUA MWANAFUNZI KWA FIMBO.

Tags
Mwanafunzi David Ngangu mwenye umri wa miaka 14 amefariki dunia baada ya kupokea kipigo kutoka kwa mwalimu wake baada ya kufeli somo la maarifa ya jamii.Mwanafunzi huyo ambaye alikua akisoma darasa la 8 katika shule ya msingi Subukia nchini Kenya alifariki saa chache baada ya kipigo.Mama mzazi wa mwanafunzi huyo alisema mtoto huyo alilalamika maumivu ya kichwa kutokana na kipigo cha mwalimu kisa ikiwa ni kufeli na kushidwa kufika wastani wa somo la maarifa ya jamii_The starndard

NCHI ZINAZOONGOZA KUA NA WANAFUNZI WENYE AKILI ZAIDI DUNIANI.

Tags
Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka Marekani na Uengereza kama vile Harvard,MIT,Stanford,Oxford, CAMBRIGDE etc.Lakini baada ya Shirika la kimataifa la Uchunguzi wa maendeleo(OECD) kuchunguza uwezo wa kusoma na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu Duniani wanafunzi walio bora zaidi wanatoka Japan na Finland na wala sio Marekani na Uengereza.Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanao hitimu kwa mujibu wa OECD ni 1.JAPAN,2.FINLAND,3.UHOLANZI,4.AUSTRALIA,5.NORWAY,6.UBELGIJI,7.NEW ZEALAND,8.ENGLAND,9.MAREKANI,10.JAMHURI YA CZECH.

SAIDI:NIMETOLEWA MACHO, SI AKILI.

Tags
Kijana aliyeshambuliwa na kutolewa macho usiku wa septemba 6 akiwa buguruni jijini Dar es salaam na habari zake kutawala katika vyombo vya habari na mitandao bw. Saidi ALLY amesema kutolewa macho sio mwisho wa maisha yake.>>Nashukuru nimepata misaada mbalimbali kutoka kwa wadau na kwa kua imekuja kama mitaji, Nitasimamia biashara hiyo nikishirikiana na mke wangu pamoja na ndugu zangu.Nina imani nitaishi mpaka siku Mungu aliyoniandikia kua nitaondoka Duniani,..Nimetolewa macho,si akili nitahakikisha vitu nilivyopewa vitatumika kwa manufaa na familia yangu na nitahakikisha inaishi maisha ya kawaida. Binafsi naamioni Mungu ndiye muwez wa yote na hakuna linalomshinda,hivyo sijakata tamaa naamini nitaona na maisha yataendelea kama kawaida.