Jumamosi, 5 Novemba 2016

KIFO CHA MUUZA SAMAKI CHAZUA MAANDAMANO MOROCCO.

Tags

Maelfu ya raia wa Morocco juzi walifanya maandamano katika miji kadhaa baada ya muuza samaki mmoja kugongwa na gali la kubebea takataka hadi kufa alipojaribu kuchukua samaki wake ambao alipokonywa na maafsa wa Polisi.
Kifo cha Maouhcine Fikri katika mji wa kaskazini wa Al Houciema siku ya Ijumaa kilizua hasira kali miongoni mwa raia katika mitandao ya kijamii.
Mfalme wa Morocco king Mohammed amewaagiza maafsa kutembelea familia ya Fikri.


EmoticonEmoticon