Jumatano, 9 Novemba 2016

AGONGA GARI LA POLISI AKIJIPIGA SELFIE

Tags

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha nchini Marekani aligongesha gari lake kwa lile la polisi wakati akijipiga selfie huku akiendesha gari.

Miranda Rader mwenye umri wa miaka 19,aliligonga gari la polisi alipokua akimtumia picha za utupu mpenzi wake kupitia mtandao wa Snapchart.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Bryan umbali wa km 160 kaskazin mwa mji wa Houston,ilisababisha mfuko wa hewa kuchomoka.
Alikamatwa kwa kushukiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa na kuachiwa kwa dhamana ya dolla 2000.


EmoticonEmoticon